Jamii FM
Huduma bure ya mama mjamzito na watoto wachanga-Makala
7 November 2024, 16:17 pm
Na Gregory Millanzi
Sera ya afya ya mama na mtoto nchini Tanzania inalenga kuboresha afya na ustawi wa wanawake wajawazito, watoto wachanga, na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Serikali ya Tanzania imekuwa ikitekeleza sera ya afya inayotoa matibabu bure kwa mama na mtoto kupitia Wizara ya Afya. Sera hii inalenga kuhakikisha kuwa wanawake wajawazito na watoto wanapata huduma za afya bila vikwazo vya kifedha.
Kituo cha Afya cha Likombe Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara kimekuwa sehemu ya utekelezaji wa sera hii na hapa tumezungumza na wanawake ambao wamefika kituoni hapa kwa ajili ya kujifungua wanaeleza hali ya huduma ilivyo.