Jamii FM

Vyama vya ushirika vyakemea kauli za upotoshaji za wanasiasa

7 April 2025, 00:00 am

Viongozi wa vyama vya Ushirika vinavyohudumia katika mikoa inayolima Korosho,ufuta na mbazi wakizungumza na vyombo vya habari(Picha na Musa Mtepa)

Tamko hili limekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za baadhi ya wanasiasa kutumia majukwaa yao kuupotosha umma juu ya mifumo ya stakadhi ghalani unavyo wakandamiza wakulima wanapouza mazao yao

Na Musa Mtepa

Wenyeviti wa vyama vikuu vya ushirika vinavyosimamia mazao ya ufuta, korosho na mbazi katika mikoa ya Lindi, Mtwara, na Ruvuma wamejitokeza kutoa tamko dhidi ya kauli zinazozungumzwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kutoona umuhimu wa matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani.

Wakizungumza na vyombo vya habari leo, Aprili 6, 2025, wenyeviti hao wamesema kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, kupitia mikutano ya hadhara, wamekuwa wakipotosha umma kwa kudai kwamba mfumo wa stakabadhi ghalani haufai kwa wakulima, jambo ambalo linapaswa kupuziwa.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika TANECU, Karim Chipola, amezungumzia manufaa ya mfumo wa stakabadhi ghalani akisema kwamba kabla ya mfumo huu, wakulima walikuwa wakikosa uhakika wa soko la mazao yao na mazingira mengine yalikuwa hayaleti tija.

Sauti ya Karim Chipola Mwenyekiti wa TANECU

Chipola amesisitiza kwamba serikali imefanya juhudi kubwa katika kusaidia wakulima, hasa katika zao la korosho, kwa kuwapa pembejeo bure na kupunguza gharama za uzalishaji huku akiwasihi viongozi wa vyama vya siasa kutoa sera zao na siyo kupotosha umma kuhusu masuala ya wakulima.

Sauti ya 2 Karim Chipola Mwenyekiti wa TANECU

Aidha, Musa Manjaula, Mwenyekiti wa chama kikuu cha Ushirika cha TAMCU, amejibu tuhuma za wanasiasa hao kuhusu tozo  zinazokatwa kwa wakulima kuwa kubwa akisema kwamba tozo zinazokatwa kwa mkulima hazi zidi shilingi mia moja tofauti na wao wanavyosema kuwa mkulima anakatwa shilingi 1000.

Pia ameendelea kusema kuwa taarifa hizo ni za kupotosha na zinapaswa kupuuzwa.

Sauti ya Musa Athumani Manjaula mwenyekiti TAMCU

Kwa upande mwingine, Al-Hajji Azam Mfaume (Jula Jula), Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha MAMCU, amesema wamepokea kwa masikitiko taarifa za baadhi ya wanasiasa kuupotosha umma kuhusu utendaji wa vyama vya ushirika na mifumo ya stakabadhi ghalani na kuwaomba wakulima kuwa makini na wanasiasa wanaotumia majukwaa yao ya kisiasa kueneza upotoshaji na kuiwataka wakulima kuelewa kwamba wanasiasa hao wanahitaji kura zao kuelekea katika uchaguzi mkuu.

Sauti ya Al-hajji Azam Mfaume Mwenyekiti wa MAMCU

Wenyeviti hawa wamesisitiza kwamba wakulima wanapaswa kuendelea kuamini mfumo wa stakabadhi ghalani na kuwa makini na taarifa potofu zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.