Mashabiki wa Simba Mtwara wafanya usafi, dua kuwaombea wachezaji
3 August 2024, 18:02 pm
Matarajio makubwa kwa mashabiki wa timu ya Simba ni kuona inafanya vizuri katika mashaindano mbalimbali itakayoshiriki timu hiyo kwa msimu wa 2024/2025 na hii ni kutokana na kufanya usajili unaotoa mategemeo makubwa kwa mashabiki wao.
Na Musa Mtepa
Mashabiki wa timu ya simba kutoka Kijiji cha Kawawa kata ya Mkunwa wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara wamesheherekea siku ya Simba(Simba day) kwa kufanya usafi katika Shule ya Msingi Kawawa,Zahanati ya Kawawa ,Msikiti mkuu wa Kawawa Pamoja na kuwafanyia Dua Wachezaji ,Viongozi na mashabiki katika kuelekea msimu mpya wa Mashindanzo.
Akizungumza na jamii fm redio leo August 3,2024 Mwenyekiti wa mashabiki hao Mohamedi Dadi Nakandu amesema katika kusheherekea siku hiyo wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali ya kijamii huku akisema kuwa hiyo ni kuonesha simba kweli ni nguvu na ndio maana wamefanya hayoi yote.
Naye Mwalimu Lyuma msemaji wa mashabiki wa Simba Kijiji cha Kawawa amesema kuwa wameamua kufanya matukio hayo wakiwa kama sehemu ya jamii ikiwa katika kurudisha fadhila kwa kuwaunga mkono yale yanayofanywa na viongozi wa kitaifa katika kusheherekea siku ya Simba day.
Himidi Bakari Namakanya Mwenyekiti wa Kijiji cha Kawawa amewashukuru mashabiki wa Simba kwa kitendo cha kufanya usafi na kutoa msaada wa fedha katika maeneo ya kijamii huku akiwataka mashabiki wat imu nyingine kuiga kitendo hicho.
Akizungumza kwa niaba ya taasisi zilizofanyiwa usafi kiongozi wa Msikiti mkuu wa Kijiji cha Kawawa Shekhe Hamisi Mfaume Palangadau amesema kupitia maandiko mwenyezi mungu ameelezea umuhimu wa kufanya usafi katika mazingira yanayo mzunguka Binadamu hivyo kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki hao ni sehemu ya kutekeleza maandiko hayo.
Baada ya kufanya usafi mashabiki hao walifanya dua ya kuwaombea Wachezaji wa Simba ,Viongozi na mashabiki wa timu hiyo iliyoenda sambamba na viburudisho mbalimbali vikiwemo chakula na Vinywaji .