Wanakijiji waomba umeme na maji.
2 November 2020, 13:07 pm
Wananchi wa kijiji cha maili kumi kata ya Mbawala Halmashauri ya wilaya ya Mtwara wameomba kupatiwa huduma ya maji na nishati ya umeme kwenye kijiji chao, hali ambayo imekuwa ikiwachelewesha maendeleo na kudumaza hali ya kijiji.
Nishati ya umeme imepita eneo la kijiji cha maili kumi lakini wananchi hawatumii nishati hiyo, na maji yamekuwa ni shida sana kwenye kijiji cha maili kumi.
Kamchochi Kamchochi ni mmoja wa mwananchi ambae ni mkazi wa kitongoji cha mbanja kijiji cha maili kumi, ameeleza namna wanavyo pitia changamoto ya maji na umeme.
Kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) ushirika wa mtwara Dayosisi ya kusini mashariki mkoani Mtwara, inajenga shule ya sekondari ya wasichana katika kitongoji cha mbanja kijiji cha maili kumi, wameomba serikali kuwapatia wananchi wa eneo hilo huduma ya maji na umeme.
Askofu Lucas Mbedule wa kanisa la KKKT ushirika wa Mtwara, ameeleza namna wananchi wanavyohitaji huduma za maji na umeme kwenye kijiji cha maili kumi.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha maili kumi amekiri nkuwepo kwa changamoto hizo na ameeleza namna wanavyoweza kuhakikisha wanazitatua kwa kushirikiana na viongozi na watendaji wa serilikali ili kumaliza changamoto hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amepokea changamoto za umeme na maji kwenyue kijiji cha maili kumi na kuhaidi kulimaliza.