Jamii FM

Vijana 25 Mtwara wapokea mikopo ya serikali

02/03/2026, 19:31

Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa mkopo wa masharti nafuu kwa vijana 25 mkoani Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Zaidi ya vijana 25 Mtwara wamenufaika na mikopo nafuu, wakiwemo wapokeaji wa pikipiki, bajaji na guta, iliyokabidhiwa na Waziri wa Vijana kwa lengo la kukuza biashara na ajira

Na Musa Mtepa

Vijana 25 mkoani Mtwara wamenufaika na mikopo yenye masharti nafuu inayosimamiwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana. Mikopo hiyo imetolewa leo, March 2, 2026, na Waziri wa Vijana, Joel Nanauka, baada ya kuzinduliwa kwa jukwaa la Vijana (Vijana Platform) mkoani Mtwara.

Waziri Nanauka amesema kuwa amewakabidhi vijana pikpiki 15, bajaji 5 na guta 5 vyenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 140, vyote ikiwa na bima zao, huku wakipewa muda wa miezi mitatu kuanza kulipa marejesho.

Sauti ya Dkt. Joel Nanauka, Waziri wa Vijana

Akizungumza kwa niaba ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dolnad Msengi, amewashauri vijana kuchangamkia fursa hiyo na kuachana na hoja za masharti magumu ya mikopo, huku akiunga mkono jitihada za Rais wa nchi katika kuwasaidia vijana kupata uchumi.

Sauti ya Dolnad Msengi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

Katibu wa chama cha waendesha boda boda na bajaji mkoa wa Mtwara, Mshamu Ali, amesema kuwa hatua ya serikali kukopesha chombo baada ya fedha italeta tija kubwa kwa vijana ikilinganishwa na ukopeshaji wa fedha pekee.

Sauti ya Mshamu Ali, Katibu wa Dereva Boda Boda na Bajaji Mtwara

Vijana wanufaika wamesema wanashukuru kwa jitihada za serikali na kueleza kuwa mikopo hiyo itawasaidia kusogeza mbele maendeleo yao binafsi na ya taifa kwa ujumla.

Sauti ya vijana wanufaika na mikopo ya vijana