Tamasha la Red Scopion La vunja rekodi mkoani Mtwara
1 September 2024, 11:06 am
“Malengo yetu sisi ni kutambulika na chama cha soka mkoani Mtwara (MTWAREFA) pamoja na kuwa timu kubwa itakayo kuwa inashiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Mtwara lakini pia kuwa timu ya kukuza na kuuza vipaji “
Na Musa Mtepa
Timu ya Red Scopion kutoka Kijiji cha Mgao August 31,2024 imeadhimisha kilele cha siku ya timu hiyo (RED SCOPION DAY) iliyohusisha utambulisho wa Wachezaji watakao tumika katika msimu wa mashindano ya 2024/25 .
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katibu msaidizi wa timu hiyo Omari Hamisi amesema malengo ya timu ni Pamoja na kujisajili katika chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mtwara (MTWAREFA ) .
Aidha Omari Hamisi amesema Pamoja na mafanikio hayo wamekuwa na changamoto mbalimbali zilinazo wakabili ikiwa Pamoja na ukosefu wa fedha za kufanyia usajili na upungufu wa vifaa vya michezo .
Kwa upande wake mgeni rasmi wa tamasha hilo mdau wa michezo ambe pia ni Diwani wa kata ya Mayanga Mhe. Arif Premji amefurahishwa na kitendo cha kualikwa katika tamasha hilo huku akitatua changamoto ya jezi na fedha za usajili zilizokuwa zinaikabili timu hiyo ili iweze kutambulika na chama cha mpira wa miguu mkoani Mtwara (MTWAREFA).
Juma Nangomwa mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Mtwara amesema uwepo wa matamasha ya kimichezo inasaidia kuleta hamasa kwa jamii kujiingiza katika michezo na kusistiza hamasa hizo kutoishia kwenye matamasha pekee .
Akielezea malengo ya tamasha la Red Scopion na timu kwa ujumla mwenyekiti wa timu hiyo Selemani Mzee Salumu amesema kuwa malengo ni kuwa timu kubwa itakayoshiriki mashindano mbalimbali Pamoja na kukuza na kuuza vipaji vya wachezaji wao.
Nao Mashabiki wameonesha kufurahia tamasha hilo na kuhitaji kuwa na mwendelezo wa uwepo wa tamasha hilo kwani kwao limekuwa sehemu ya sikukuu.
Tamasha la Red scopion limefanyika jana August 31,2024 katika Kijiji cha Mgao kilichopo kata ya Naumbu Halmashauri ya Mtwara vijijini mkoani Mtwara ambapo katika tamasha hilo kulikuwepo na burudani mbalimbali kama vile Muziki kutoka Msanii LastBorn kutoka Kijiji cha Mgao aliyetambulisha wimbo wake mpya kwenye tamasha hilo,Dogo Chidy msanii anae tamba na wimbo wa Usijali ,Wachezaji Muziki kutoka katika Kijiji cha Mgao na utambulisho wa wachezaji watakao shiriki mashindano mbalimbali katika msimu wa 2024/25.
Aidha katika kuhitimisha tamasha hilo kulifanyika mchezo wa mpira wa miguu katika timu mwenyeji ya Red scopion fc na Jordan fc kutoka katika Kijiji cha Mnima ambapo mwenyeji alikubali kichapo cha goli moja bila.