

1 April 2025, 12:43 pm
Maonesho hayo yatafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chikongola Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo bidhaa zitahusisha zilizotengenezwa katika mafunzo yaliyoratibiwa na ADEA kwa kufadhiliwa na Alwaleed na Unesco.
Na Musa Mtepa
Hiki ni kipindi kilichofanyika katika Studio za Jamii fm redio kilicholenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika maonesho ya bidhaa za sanaa katika viwanja vya shule ya msingi Chikongola Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo katika maonesho hayo zitaoneshwa bidhaa mbalimbali zilizozalishwa na wanafunzi waliopata mafunzo kutoka shirika la ADEA kwa kufadhiliwa na UNESCO na Alwaleed yakiwa na lengo la kuboresha bidhaa zinazotengenezwa na utangazaji wa masoko kwa wanasanaa hao.