Mpanda FM
Mpanda FM
20 November 2021, 1:06 pm
Baadhi ya wananchi manispaa ya mpanda mkoani katavi wamekuwa na maoni tofauti juu ya katazo la madalali wa nyumba kupewa kodi ya mwezi mmoja. wakizungumza na mpanda radio fm wananchi hao wameleza kufurahishwa kwa marufuku hiyo huku wengine wakionesha kutoridhishwa…
20 November 2021, 12:30 pm
Mkuu wa wilaya ya mpanda Jamila Yusuph amewaagiza wakurugenzi wa manispaa ya mpanda na halmashauri ya nsimbo kusimamia miradi ya maendeleo ili inapokamilika iwe na ubora unaoendana na thamani ya pesa iliyotolewa. Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya…
20 November 2021, 12:25 pm
Hifadhi ya taifa mkoani katavi inatajwa kuwa moja ya hifadhi inayoongoza kuwa na viboko wengi afrika huku idadi ya viboko hao ikikadiriwa kuwa ni zaid ya milioni mbili . Hayo yamebainishwa na muongoza watalii katika hifadhi hiyo God listern Isaya…
20 November 2021, 11:45 am
Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka viongozi wa serikali kutokuwa chanzo cha kukumbatia uharifu katika jamii. Akizungumza na Mpanda Radio Fm amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya viongozi wa serikali kutumia nafasi zao za kazi kuwatetea waharifu…
20 November 2021, 11:35 am
Serikali mkoani katavi imekuja na mpango harakishi na shirikishi wa kutoa huduma mkoba ya uviko19 ambavyo itawasaidia wananchi kupata chanjo hiyo popote pale walipo. Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkao wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ambapo ameeleza kuwa wamekuja na…
20 November 2021, 10:52 am
Madereva wa vyombo vya moto mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria na taratibu zote za usalama barabarani. Wito huo umetolewa mapema leo na Sanjeti Jofrey Britoni wakati akizungumza na kituo hiki na kubainisha kumekuwa na madereva wanaovunja na kukaidi kufuata utaratibu…
20 November 2021, 10:44 am
Wananchi mkoani katavi wameshauliwa kubadili mtindo wa maisha ili kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo. Kauli hiyo imetolewa na daktari wa idara ya magonjwa yasiyoambukiza kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa katavi dokta Daniford Mbohilu…
20 November 2021, 10:32 am
Mamlaka ya mapato wilaya ya mpanda Mkoani katavi imefanikiwa kukusanya shilingi milioni mia tatu sabini na moja kwa kipindi cha mwezi augusti sawa na asilimia themanini na tisa ya lengo lililopangwa. Kauli hiyo imetolewa na afisa kodi daraja la kwanza…
19 November 2021, 12:41 pm
Jumla ya wateja 602 wa huduma ya maji wafutiwa madeni yao na mamlaka ya maji safi na mazingira Manispaa ya Mpanda Muwasa baada ya bodi kujilidhisha kuwepo kwa changamoto ya madeni hayo Akizungumza na Mpanda Redio FM afisa biashara wa…
19 November 2021, 12:33 pm
Wananchi wa wilaya ya mpanda mkoani katavi wameiomba serikali kupitia idara ya uhamiaji kutoa elimu ya uraia ili kuwajengea wananchi uelewa katika masuala ya uraia. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mpanda redio baadhi ya wananchi wamesema hawana elimu ya kutosha…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
