Mpanda FM
Mpanda FM
8 June 2022, 3:47 pm
Wanawake katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kujishughulisha ili waweze kujikwamua na umaskini. Wakizungumza na mpanda radio fm wanawake ambao wanajishughulisha na upetaji wa pumba na kujipatia chenga za mchele na kisha kuziuza wameeleza namna kazi hiyo…
8 June 2022, 3:45 pm
Wanachama wa Chama cha wafugaji wa ngombe wa maziwa cha Kashauriri Livestock Keepers kilichopo Wilayani Mpanda wameomba kuwezeshwa na taasisi za fedha kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kutoa fursa ya ajira kwa jamii. Wakizungumuza wakati wa kilele cha maadhimisho…
8 June 2022, 3:42 pm
Baadhi ya wazazi na walezi mkoani katavi wameshauriwa kuwalea watoto katika misingi bora ili kuepuka janga la watoto wa mitaani na mmomonyoko wa maadili. Wakizungumza na mpanda fm baadhi ya wazazi hao wamesema kuwa hali duni ya maisha ndio sababu…
8 June 2022, 3:41 pm
Kata ya kasokola iliyopo manispaa ya mpanda inakabiliwa na upungufu wa miundo mbinu wa madarasa na madawati katika shule za msingi na sekondari. akizungumza na Mpanda radio fm katika kipindi Cha kumekucha Tanzania Diwani wa kasokola Crisant Andrea Mwanawima amesema…
8 June 2022, 3:34 pm
Naibu waziri wa kilimo na uvuvi Abdala Ulega Amezitaka jamii mkoani Katavi kutumia mafundisho waliyoyapata katika maadhimisho ya wiki ya maziwa ili kuleta mabadiliko katika sekta ya maziwa nchini. Akizungumza wakati wa kufunga wiki ya maziwa mkoani hapa Ulega amesema…
26 May 2022, 1:27 pm
Vijiji saba vilivyopo ndani ya Wilaya ya Mpanda mkoani katavi vitanufaika na upatikanaji wa maji kupitia Wakala wa maji na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) katika mwaka wa fedha 2022/23. Akizungumza na Mpanda Radio FM Meneja wa RUWASA Wilayani Mpanda…
25 May 2022, 4:23 pm
Jamii mkoani katavi imeaswa kushirikiana na tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuku katika kutokomeza vitendo vyote vya rushwa mkoani hapa. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Takukuru Mkoani katavi Festo Mdede wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa…
25 May 2022, 4:17 pm
Mafisa wa polisi mkoani katavi wametakiwa kufanya kazi kwa ubora huku wakizingatia nidham usiri na uadili katika kutoa huduma kwa wananchi. hayo yameelezwa na kamanda wa jeshi la polisi nnchi IGP Simon Siro katika uzinduzi wa zahanati ya polisi mkoani…
23 May 2022, 2:34 pm
Jumla ya shilingi million 470 zimetolewa katika wilaya ya Tanganyika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya msingi katika shule maalumu ya msakila. Akizungumza na Mpanda radio fm kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Tanganyika Betuel Luhega wakati wa ziara ya…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
