Mpanda FM
Mpanda FM
29 November 2022, 8:02 pm
KATAVI Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza wakurugenzi wa mkoa, kuhakikisha wanafunzi wote watakaojiunga na msimu mpya wa masomo mwaka 2023 wanapata chakula wakiwa shuleni . Agizo hilo amelitoa wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa…
28 November 2022, 7:34 pm
MPANDA Kata ya Kawajense na Nsemlwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa madawati na vyumba vya madarasa katika Shule za msingi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mpanda Radio fm diwani wa kata ya Kawajense Uwezo…
26 November 2022, 7:50 pm
KATAVI Serikali mkoani Katavi imesema imejipanga katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kutoa elimu kwa wananchi. Hayo yamesemwa na afisa maendeleo ya jamii Joshua Sankala alipokuwa kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya siku 16…
26 November 2022, 6:56 am
MPANDA Wafanyabiashara kata ya Kashaulili manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kufanya usafi katika maeneo yao ya biashara ikiwa ni pamoja na kuchukuwa tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko. Wito huo umetolewa na Afisa mtendaji wa Kata ya Kashaulili Merry…
26 November 2022, 6:17 am
MPANDA Katika kuadhimisha wiki ya Mlipa kodi Mamlaka ya ukusanyaji mapato [TRA] mkoani Katavi wametembelea hospitali mpya ya mkoa na kufanya usafi pamoja na kutoa msaada kwa wagonjwa. Akizungumza wakati wa zoezi hilo Meneja wa mamlaka ya ukusanyaji mapato mkoa…
25 November 2022, 4:55 am
KATAVI Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 17.254 kwaajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania Tanroads mkoa wa Katavi Injinia Martin Mwakabende amesema mkoa…
25 November 2022, 4:37 am
MPANDA Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua hoza Mrindoko amewaagiza wakuu wa wilaya , kuhakikisha wananchi wote waliovamia maeneo ya hifadhi pamoja na vyanzo vya maji wanaondoka katika maeneo hayo. Agizo hilo amelitoa katika kikao cha 19 cha kamati ya…
23 November 2022, 6:38 pm
MPANDA Wafugaji kata ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuondoa mifugo yao na kufugia nje ya mji. Katazo hilo limetolewa na Afisa mtendaji wa kata ya Kashaulili Merry Ngomarufu ambapo amesema wafugaji wote wenye mifugo iliyopo katika kata…
23 November 2022, 6:19 pm
NSEMLWA Imeelezwa kuwa kukosekana kwa gari la kuzolea taka katika kata ya Nsemlwa Halmashauri Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi kunachangia baadhi ya wanchi kutupa takataka kwenye mitaro ya kupitishia maji. Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wa kata hiyo…
23 November 2022, 5:47 pm
MPANDA Wafanyabiashara Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kutoa ushuru kikamilifu,ili fedha hizo ziweze kusaidia kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwamo ya elimu na afya. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sofia Kumbuli ambapo amesema kuwa swala…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
