Mpanda FM
Mpanda FM
17 January 2023, 5:39 pm
KATAVI Wananchi manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewaomba Wauzaji wa vyakula migahawani kuzingatia kanuni za usafi ili kuepukana na Magonjwa ya milipuko yanayoweza kuwapata Wateja. Wakizungumza na Mpanda Radio wamesema kuwa kuna baadhi ya wahudumu wa migahawa hawazingazii kanuni za…
17 January 2023, 5:33 pm
KATAVI Wananchi Mkoani Katavi wameombwa kujitokeza katika uzinduzi wa jengo la mahakama ya hakimu mkazi mkoani Katavi . Wito huo umetolewa na Afisa Habari wa mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Katavi Wakili James Kapele ambapo amesema uzinduzi huo utaambatana…
17 January 2023, 4:55 pm
MPANDA Wananchi wa Mtaa wa Msasani Kata ya Mpanda Hotel wamelalamikia kukosekana kwa maji safi na salama kwa matumizi yao ya kila siku. Wakizungumza na Mpanda Radio Fm Wamedai changamoto imekua ni ya kudumu kutokana na mabomba kuharibika mara kwa…
15 December 2022, 9:56 pm
MLELE Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amezigawa nyumba Kwa watumishi wa serikali katika halmashauri ya wilaya ya Mlele kutokana na kutokaliwa na watu na kuharibika. Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa halmashauri hiyo ambapo…
15 December 2022, 10:24 am
MLELE Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kuangalia upya utolewaji wa vibali vya ukataji miti ili kuthibiti ukataji miti na kutunza mazingira. Akizungumza na watumishi wa umma katika halmashauri ya…
15 December 2022, 10:17 am
TANGANYIKA Katika kuimarisha huduma za kimahakama mkoani Katavi Serikali imejipanga kujenga majengo mapya katika makao makuu ya tarafa zote wilayani Tanganyika. Hayo yamesemwa na naibu waziri wa katiba na sheria Geofrey Pinda wakati wa ziara ya waziri Mkuu Kassim Majaliwa…
14 December 2022, 5:43 pm
MLELE Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza halmashauri ya wilaya ya mlele katika makusanyo ya mwezi wa 10 hadi 12 waanze ujenzi wa shule nyingine ya sekondari ili kupunguza mlundikano wa wanafunzi uliopo katika shule ya sekondari Majimoto. Akizungumza baada ya…
13 December 2022, 6:50 pm
KATAVI WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amemuagiza kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa {TAKUKURU} mkoa wa Katavi awachunguze watumishi wawili akiwemo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Mpanda {MUWASA}, Hussein Nyemba kwa tuhuma za kukiuka taratibu za…
13 December 2022, 9:23 am
MPANDA Mamlaka ya maji manispaa ya mpanda Ruwasa imeagizwa kuhakikisha mradi wa maji katika kata ya mwamkulu unakamilika ili kupunguza adha kwa wananchi. Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph wakati akifanya ziara ya ukaguzi wa…
13 December 2022, 9:18 am
KATAVI Waziri Mkuu Wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa amesema kiasi cha fedha cha shillingi Bilioni 150 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo kwa wakulima ili wapate mbolea na dawa Mkoani Katavi. Ameyasema hayo alipokuwa…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
