Mpanda FM
Mpanda FM
15 March 2023, 11:57 am
MPANDA Diwani wa kata ya magamba ametoa siku mbili kwa Uongozi wa kikundi cha kagera group kuwasilisha taarifa ya uendeshaji wa kikundi hicho ili kurahisisha agenda ya uchaguzi kuziba nafasi za viongozi waliovuliwa nyadhifa zao. Agizo hilo limetolewa na diwani…
15 March 2023, 11:48 am
MPANDA Katika kuazimisha kipindi cha mfungo wa kwaresima parokia ya kanisa katoliki Katumba imetoa msaada wa zaidi ya laki saba kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaotoka katika mazingira magumu kilichopo kata ya nsemlwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.…
14 March 2023, 7:35 pm
KATAVI Waandishi wa Habari mkoani Katavi wamemuomba mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko kutatua changamoto zinazowakabili , ikiwemo kukosa bima ya afya, kukosa mikopo na kukosa ushirikiano kwa baadhi ya wakuu wa idara. Wakizungumza mbele ya mkuu wa…
14 March 2023, 7:18 pm
KATAVI Wadau wa maendeleo Mkoani katavi wameombwa kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Makanyagio iliyopo Manispaa ya Mpanda. Afisa mtendaji wa Kata ya Makanyagio Maiko Ndaile amesema kuwa tayari wameanza ujenzi kwa michango ya wananchi wakishirikiana na Viongozi ndani…
13 March 2023, 9:47 am
KATAVI Jumla ya Tofali Elfu kumi zimepokelewa na kamati ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Msasasani iliyopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Kwa ajili ya kuanza ujenzi wa shule. Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule Celestine Shemtange ameiambia Mpanda…
13 March 2023, 9:39 am
MPANDA Baadhi ya viongozi wa kikundi cha Kagera group wamevuliwa nyazifa zao kutokana na mgogoro unaoendelea katika kijiji cha Dirifu Na wachimbaji wadogo huku nafasi zao zikitarajiwa kuzibwa hivi karibuni. Akizungumza wakati wa kutoa maamuzi hayo diwani wa kata ya…
9 March 2023, 1:23 pm
KATAVI Kutokuwa na uhuru wa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo,rushwa,na kutokujua sheria zimetajwa kuwa ni changamoto zinazowakabiri wanawake. Akisoma Risala , Bi. Chiku Peter na kuwawakilisha wanawake katika kusherehekea siku ya wanawake duniani iliyofanyika Machi 8 mwaka huu amesema kuwa …
9 March 2023, 1:18 pm
NSIMBO Baadhi ya wananchi wametoa maoni mseto kutokana na tukio la mtoto mchanga kutupwa katika shimo la choo kitongoji cha Isagala kijiji cha Uruwila Hamshauri ya Nsimbo Mkoani Katavi. Wakizungumza na Mpanda Redio Fm kwa nyakati tofauti wameviomba vyombo vya…
9 March 2023, 1:15 pm
KATAVI Miili ya watu 9 waliofariki katika ajali ya basi ya kampuni ya Kombas iliyotokea march 6 katika mlima Nkondwe halmashauri ya wilaya Tanganyika mkoani Katavi imeagwa katika hospital ya manispaa ya Mpanda . Akizungumza wakati wa zoezi la kuaga…
9 March 2023, 1:12 pm
KATAVI Watu Wenye ulemavu Mkoani Katavi wameshauriwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia mbili inayotolewa na serikali kupitia halmashauri zote nchini. Katibu wa Chama cha watu wenye ulemavu Mkoa wa Katavi Godfrey Sadala ameiambia Mpanda Radio kuwa watu wenye ulemavu…
Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.
Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.
Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.
Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.
