Mpanda FM

Recent posts

30 May 2023, 10:19 am

Sauti ya Katavi (Matukio)

MPANDA Wafanyabiashara wilaya Mpanda mkoani Katavi wameishutumu Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Katavi kuwa ni moja ya chanzo cha  kufirisika kwa mitaji yao. Wafanyabiashara hao wamebainisha hayo katika kikao kilichoandaliwa na mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza…

30 May 2023, 10:10 am

Wakurugenzi watenge bajeti sekta ya michezo

MPANDA Katibu tawala wa mkoa wa Katavi Hassan Rugwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha wanatenga bajeti ili kuwezesha sekta ya michezo. Akizungumza wakati wa kufungwa kwa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za msingi…

30 May 2023, 10:06 am

Wakulima wa pamba Tongwe walia na bei ya zao hilo

KATAVI Wakulima wa zao la pamba kijiji cha Vikonge kata ya Tongwe halmshauri ya wilaya ya Tanganyika wameiomba serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuongeza bei ya zao hilo. Wakizungumza katika uzinduzi wa soko la mauzo ya zao la pamba katika…

26 May 2023, 10:57 am

Sauti ya Katavi (Matukio)

MPANDA Wadau wanaozalisha mazao yatokanayo na mifugo Mkoa wa Katavi, wametakiwa kufuata sheria, ikiwemo kuboresha usafi katika mabucha, na kuepuka matumizi ya magogo na vyuma vyenye kutu ili kulinda afya ya walaji.  Afisa Mfawidhi wa Bodi ya Nyama Kanda ya…

26 May 2023, 10:47 am

TAKUKURU yabaini mapungufu wilaya ya Tanganyika

KATAVI Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi imebaini kuwepo kwa mapungufu yakiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa miradi, ukiukwaji wa mikataba na ucheleweshaji wa kukamilisha miradi mitano katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika mkoani hapa.…

26 May 2023, 10:42 am

Magogo yapigwa marufuku buchani

MPANDA Wadau wanaozalisha mazao yatokanayo na mifugo mkoa wa Katavi , wametakiwa kufuata sheria, ikiwemo kuboresha usafi katika mabucha, na kuepuka matumizi ya magogo na vyuma vyenye kutu ili kulinda afya ya walaji. Maagizo hayo yametolewa na Afisa Mfawidhi wa…

26 May 2023, 10:32 am

Wananchi washauriwa kufanya usafi wa kinywa na meno

MPANDA Jamii Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imeshauriwa kufanya vipimo vya meno, kufanya usafi wa kinywa kwa kuzingatia muda, kuepuka matumizi holela ya dawa zisizo za kitabibu ili kuepukana na magonjwa ya meno na kinywa kutoa harufu mbaya. Ushauri huo…

26 May 2023, 10:26 am

CHADEMA na Katiba Mpya kabla ya uchaguzi

KATAVI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaendelea kusimamia misingi ya chama hicho kwa kutetea haki, uhuru, na demokrasia kwa wanachama wa chama hicho na wananchi wa taifa kwa ujumla. Akiwahutubia wanachama wa chama hicho katika uzinduzi wa…

23 May 2023, 8:02 pm

Sauti ya Katavi (Matukio)

MPANDA Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani hapa Katavi wameshauriwa kubadilisha mfumo wa maisha katika vyakula wanavyokula ikiwa ni pamoja na kujenga desturi ya kufanya mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dr Paulo Swakala ambaye ni Mganga Mkuu…

23 May 2023, 7:32 pm

TAKUKURU yafichua maduka yanayouza viuatilifu mali ya serikali

KATAVI Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Katavi imefanikiwa kufichua maduka yanayouza viuatilifu ambavyo ni mali ya serikali chini ya usimamizi wa bodi ya pamba. Hayo yamesemwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Katavi Faustine Maijo…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.