Mpanda FM

Recent posts

5 May 2023, 5:00 am

Klabu za Elimu Kunufaisha Wanafunzi

MPANDA Uwepo wa Klabu za kutoa elimu mashuleni imetajwa kuwa moja ya sababu ambazo zinamsadia mwanafunzi katika masomo na Maisha yake kwa jamii Baadhi ya wanafunzi katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema wamekuwa wakipata elimu ya ugonjwa…

2 May 2023, 9:18 pm

Wananchi Waomba Elimu ya Lishe kwa Wajawazito

KATAVI. Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameomba kupatiwa elimu juu ya umuhimu wa lishe bora kwa mama mjamzito. Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamesema hawapatiwi elimu juu ya lishe bora kwa mama mjamzito zaidi ya…

2 May 2023, 9:41 am

Katavi yapanda miti milioni 6 tangu mwezi Februari

NSIMBO Serikali mkoa wa Katavi imesema miti milioni sita imepandwa toka mwezi wa Februari mwaka huu katika halmashauri za mkoa wa Katavi. Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amebainisha hayo wakati akizungumnza na wananchi wa Kijiji Cha Isinde halmashauri…

2 May 2023, 9:35 am

Madereva Bajaji Walalamikia Usumbufu Stendi ya Tanganyika

KATAVI Baadhi ya madereva Bajaji wanaofanya safari kutoka Mpanda mjini kuelekea wilaya ya Tanganyika wamelalamikia usumbufu wa kulazimishwa kuingia stendi ili kutoa ushuru. Wakizungumza na Mpanda Radio FM madereva wamesema awali walikuwa wakifanya safari bila kulazimika kuingia stendi hiyo huku…

27 April 2023, 5:58 pm

Surua Yawatia Hofu Wakazi wa Dirifu

MPANDA Wananchi wa kijiji cha Dirifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwapa elimu juu ya ugojwa wa surua ambao unasambaa katika kijiji hicho. Wakizungumza na Mpanda redio fm wananchi wameainisha kuwa baadhi ya familia katika…

27 April 2023, 5:52 pm

Mpunga Hatarini Kuharibika kwa Mvua

MPANDA Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mwamkulu manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamehofia kuharibika kwa zao la mpunga uliopo shambani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Wakizungumza na kituo hiki wamesema kuwa kuna hatari ya kupoteza mazao ya mpunga kutokana…

27 April 2023, 8:19 am

Wananchi 53 Mpanda Wanufaika na Mafunzo ya Ujasiriamali

MPANDA Jumla ya wananchi 53 manispaa ya Mpanda mkoani katavi ikiwamo wanawake pamoja na vijana wamenufaika na mafunzo ya ujasiliamali yaliyowezeshwa na Diwani wa viti maalumu kata ya majengo kupitia chama cha mapinduzi CCM lengo likiwa ni kuwapa ujuzi na…

22 April 2023, 9:45 am

Buswelu: Jipangeni Kukusanya Mapato Yanayopotea

TANGANYIKA Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ametoa maelekezo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Tanganyika kuangalia namna bora ya ukusanyaji wa mapato katika kipindi hiki cha mavuno. Maelekezo hayo ameyatoa wakati wa kikao cha baraza la madiwani wilaya ya…

22 April 2023, 9:38 am

Ulinzi Waimarishwa Sikukuu za Eid El Fitr

KATAVI Katika kuelekea sikukuu ya Eid El Fitri Jeshi la polisi mkoa wa Katavi limepanga kuimarisha ulinzi ili kupunguza uvunjifu wa sheria kipindi cha sikukuu. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Katavi Ali Makame Hamad…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.