Mpanda FM

Recent posts

16 June 2023, 7:11 pm

Wadau wa nyama 30 watozwa faini Katavi

KATAVI. Zaidi ya shilingi milioni 3 zimetozwa kwa wadau wa nyama 30 kati ya 81 baada ya kupigwa faini kwa makosa kama ubovu wa miundombinu katika machinjio mkoani Katavi. Akizungumza na Mpanda Redio FM Afisa mfawidhi wa nyama kanda ya…

12 June 2023, 2:40 pm

TCRA yatoa mafunzo Mpanda Radio Fm

MPANDA Vyombo vya habari mkoani Katavi vimetakiwa kufuata sheria, kanuni na miongozo pamoja na kulinda haki ya mtoto na kutokutoa vipindi vyenye maudhui yenye lugha ya matusi. Hayo yamebainishwa na Josephine Ndeje afisa mahusiano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA]…

10 June 2023, 3:35 pm

Mpanda: Wananchi waomba mchakato TASAF upitiwe upya

MPANDA Wananchi wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kupitia upya mchakato wa upatikanaji wa kaya maskini ili kuuwezesha mpango wa kunusuru kaya maskini unafika kwa walengwa kama ilivyokusudiwa. Wakizungumza na Mpanda Radio fm wananchi hao wameonyesha kutoridhishwa na…

10 June 2023, 3:32 pm

Jamii yaaswa kutofumbia macho vitendo vya ukatili

MPANDA Kukosa elimu ya ukatili wa kimwili kumetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea watu wa karibu kushindwa kuripoti matukio ya ukatili wa kimwili kipindi yanapotokea. Hayo yamebainishwa na wakazi wa manispaa ya Mpanda wakati wakizungumza na kituo hiki na kuongeza…

10 June 2023, 3:29 pm

Mashindano UMISETA yafungwa Katavi

KATAVI Wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanasimamia michezo na kuzitengea bajeti idara zote za michezo katika maeneo yao. Maagizo hayo yametolewa na katibu tawala wa mkoa wa Katavi Hassan Rugwa wakati akifunga mashindano ya Umoja wa Michezo…

7 June 2023, 5:40 pm

Sauti ya Katavi (Matukio)

MPANDA. Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya usalama wa chakula diniani mkoa wa katavi ni miongoni mwa mikoa Tanzania inayozalisha mazao ya chakula kwa wingi licha ya kukabiliwa na changamoto ya utapia mlo na udumavu kwa watoto. Kufuatia siku…

7 June 2023, 5:36 pm

Katavi: Wawili jela miaka mitatu mauaji bila kukusudia

KATAVI Watu wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kila mmoja mara baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia mkoani Katavi huku watu wengine wanne wakienda jela kwa makosa ya wizi. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa…

7 June 2023, 10:59 am

Mafunzo uongozi yatolewa Katavi

KATAVI Maafisa tarafa na watendaji wa kata mkoa wa Katavi wametakiwa kutekeleza majukumu ya serikali katika maeneo yao. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Katavi wakati wa utolewaji wa mafunzo ya…

7 June 2023, 10:54 am

Sauti ya Katavi (Matukio)

KATAVI Watu wawili  Mkoani Katavi wamehukumiwa kifungo cha Miaka Mitatu kila mmoja jela kwa tuhuma za kuua bila kukusudia huku wengine Wanne wakienda Jela kwa makosa ya Wizi. Mwandishi wa Mpanda Radio Henry Mwakifuna amefika ofisi za Kamanda wa Polisi…

7 June 2023, 10:28 am

Dirifu walia ukosefu huduma ya maji

MPANDA Wananchi wa kijiji cha Dirifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamezitaka mamlaka za maji kupitia serikali ya mkoa kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa kipindi kirefu. Hayo yamewasilishwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.