Mpanda FM

Recent posts

24 July 2023, 10:09 am

Uelewa bado mdogo Katavi mradi wa BBT

KATAVI. Wananchi na wakulima mkoani Katavi wameonesha kutokuwa na uelewa wowote kuhusiana na mradi wa serikali unaoratibiwa na Wizara ya Kilimo, mradi wa jenga leo kesho iliyo bora maarufu kama (BBT). Wakizungumza na Mpanda Redio FM wameeleza kuwa ni vema…

24 July 2023, 10:06 am

Hati miliki za ardhi zatolewa Tanganyika

TANGANYIKA Taasisi ya Jen Goodall kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Tanganyika chini ya mradi wa uhifadhi wa maliasili Tanzania wamefanya uzinduzi na ugawaji wa hati miliki katika kijiji cha Vikonge halmashauri yaTanganyika. Akizungumza katika uzinduzi huo Naibu Mkurugenzi…

17 July 2023, 10:17 am

Special Talent Search STS

Inyonga imetoa washindi watatu katika mashindano ya kusaka vipaji STS yaliyofanyika Julai 15 Katika viwanja vya shule ya msingi Inyonga. #mpandaradiofm97.0 #katavists

17 July 2023, 10:15 am

Shule ya Makomelo Kupunguza Adha ya Mrundikano Shuleni

KATAVI Adha ya Wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Kitongoji cha Songambele Kijiji cha Tumaini Kata ya Itenka kutembea Umbali wa Kilomita 9 kupata Elimu shule ya Msingi Itenka inatarajiwa kuisha kuanzia Mwezi Agosti pindi itakapokamilika Shule mpya ya Makomelo.…

17 July 2023, 10:09 am

Nimonia kwa Watoto Inaepukika

MPANDA Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Paul Swakala amewashauri wazazi na walezi kuwakinga Watoto na baridi kwa lengo la kuwaepusha na magonjwa yatokanayo na baridi ikiwemo NIMONIA . Ushauri huo ameutoa wakati akiongea na Mpanda Radio fm ofisini kwake…

13 July 2023, 10:10 am

Afunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja

MPANDA Athumani Juma Mohamed Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amefunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo. Akizungumzia ndoa yake Yengayenga…

10 July 2023, 10:33 am

Mawasiliano kuimarika Katavi

MPANDA Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, kupitia mradi wa Tanzania ya Kidigitali inatarajia kujenga minara ya mawasiliano katika mkoa wa Katavi ili kuimarisha mawasiliano kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi mkoani humo. Hayo amesema na Naibu…

10 July 2023, 10:30 am

Kituo cha afya Kazima chaanza kutoa huduma

MPANDA Mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe Mwanamvua Mrindoko amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi halmashauri ya manispaa ya Mpanda. Moja ya miradi iliyotembelewa ni kituo cha afya Kazima kilichojengwa kwa fedha za tozo za miamala ya simu. Katika ziara…

10 July 2023, 10:24 am

Katavi: Maji safi na salama bado kilio Kamlenga

KATAVI Wananchi wa kitongoji cha Kamlenga kijiji cha Sibwesa halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi wameiomba serikali iwasaidie upatikanaji wa maji safi na salama ili kuepukana na magonjwa ya tumbo. Wakizungumza na Mpanda Radio fm wananchi hao wamesema kuwa wanatembea umbali…

30 June 2023, 10:34 am

Marufuku kuacha moto ndani ya duka

KATAVI Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Katavi linaendelea na uchunguzi wa ajali ya moto iliyotokea katika duka moja soko kuu Mpanda huku likionya wanaoacha moto wakati wa kufunga maduka yao. Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.