Mpanda FM

Recent posts

30 June 2023, 10:24 am

Katavi: Kusafirisha asali lazima kibali

KATAVI Wafanyabiashara wa mazao ya nyuki manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wemetakiwa kufuata taratibu na sheria za usafirishaji wa mazao ya nyuki ikiwamo kuwa na vibali vya usafirishaji. Mpanda Radio Fm imezungumza na wafanyabiashara wanaojihusisha na uuzaji wa asali ili…

30 June 2023, 10:21 am

Mpanda: Uchimbaji madini uzingatie maeneo tengefu

MPANDA Wananchi wa kijiji cha Dirifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameshauriwa kutunza mazingira na kufanya shughuli za uchimbaji madini kwenye maeneo yaliyotengwa. Hayo yamesema na mtendaji wa kijiji hicho Evelius Mathayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa…

30 June 2023, 10:17 am

Mpanda: Mwanafunzi atekwa, polisi yawadaka watuhumiwa

KATAVI Watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi kwa kutuhuma za kumteka mtoto mdogo wa kike (9) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Mizengo Pinda katika manispaa ya Mpanda. Kaimu Kamanda wa Polisi wa…

30 June 2023, 10:07 am

Mpimbwe: Juhudi ziongezwe uhifadhi mazingira

MLELE Jamii katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi imeaswa kuongeza juhudi katika kuhifadhi mazingira. Akifungua mkutano wa mwaka wa Jumuiya za watumia maji ngazi ya Jamii zilizo chini ya wakala wa usambazaji Maji na usafi na mazingira…

16 June 2023, 7:24 pm

Wananchi Kilimani waneemeka ufugaji samaki

MPANDA Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kilimani kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamekuwa na maoni mseto kutokana na fursa za ufugaji wa samaki zinazofanywa na mwekezaji Injinia Ismail Nassoro. Wakizungumza na kituo hiki wananchi wamesema kupitia…

16 June 2023, 7:22 pm

Wakazi Dirifu waomba utaratibu kusomewa mapato, matumizi

MPANDA Wakazi wa kijiji cha Dirifu manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi wamewataka viongozi wa kijiji hicho kuwa na utaratibu wa kuwasomewa mapato na matumizi ili kuongeza uwajibikaji kwa wananchi. Wakizungumza katika mkutano wa hadhara, wananchi hao wamesema kuwa kumekuwa…

16 June 2023, 7:20 pm

Wananchi Dilifu wajitokeza kuchangia damu

MPANDA Wananchi wa kijiji cha Dilifu kata ya Magamba manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamejitokeza kuchangia damu katika kuadhimisha siku ya Wachangiaji damu Duniani. Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wananchi hao wamesema kuwa wameamua kutoa damu ili kuweza kuwasaidia wanaohitaji…

16 June 2023, 7:15 pm

Mwanafunzi kidato cha pili abakwa Katavi

MPANDA Mwanafunzi wa kidato cha pili mkazi wa Misengereni kata ya Ilembo mKoani Katavi amebakwa na mwanaume ambaye aliingia ndani ya nyumba kwa kuruka ukuta wakiwa wamelala . Mama mdogo wa binti huyo ameeleza namna tukio hilo lilivyokuwa mara baada…

16 June 2023, 7:11 pm

Wadau wa nyama 30 watozwa faini Katavi

KATAVI. Zaidi ya shilingi milioni 3 zimetozwa kwa wadau wa nyama 30 kati ya 81 baada ya kupigwa faini kwa makosa kama ubovu wa miundombinu katika machinjio mkoani Katavi. Akizungumza na Mpanda Redio FM Afisa mfawidhi wa nyama kanda ya…

12 June 2023, 2:40 pm

TCRA yatoa mafunzo Mpanda Radio Fm

MPANDA Vyombo vya habari mkoani Katavi vimetakiwa kufuata sheria, kanuni na miongozo pamoja na kulinda haki ya mtoto na kutokutoa vipindi vyenye maudhui yenye lugha ya matusi. Hayo yamebainishwa na Josephine Ndeje afisa mahusiano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania [TCRA]…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.