Mpanda FM

Recent posts

18 March 2024, 2:08 pm

Waliofyekewa mahindi Katavi washukuru mchango wa Mpanda Radio FM

“Wakulima hao walifyekewa mahindi baada ya kile kilichosemwa ni ukiukwaji wa sheria ya kulima mazao marefu kwa Manispaa ya Mpanda katika maeneo yaliyokatazwa, lakini yaliacha maswali baada ya kadhia hiyo kuwakumba wakulima watatu pekee huku maeneo mengine mazao yakiendelea kuachwa“…

15 March 2024, 6:01 pm

KATAVI, TMDA Yabaini Ongezeko la Ugonjwa wa Figo

“Kuna changamoto ya Ini na Figo kushindwa kufanya kazi, na Saratani kuongezeka katika Jamii Yanayosababishwa na  matumizi mabaya ya dawa kwa baadhi ya Wananchi” Picha na Mtandao Na Samwel Mbugi-katavi Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA] kutoka makao Makuu…

15 March 2024, 3:18 pm

KATAVI,Waandishi Tumieni Kalamu kwa Weledi

“Wandishi wa habari Mkoani Katavi wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ili kuepusha sintofahamu kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025″. Picha na Ben Gadau Na Ben Gadau-katavi Wandishi wa habari Mkoani Katavi wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia miiko…

7 March 2024, 3:29 pm

Wanawake Katavi wapanda miti kutunza mazingira

“Miti hiyo inayopandwa itakuwa ni kumbukumbu ya maadhimisho ya siku ya mwanamke mwaka huu lakini pia ni sehemu uendelezaji wa utunzaji mazingira mkoani hapa“ Na Deus Daud-katavi Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani  manispaa ya Mpanda imefanya…

7 March 2024, 3:09 pm

MPANDA,Homa ya Ini Yaongezeka kwa Kasi

“Daktari wa Manispaa ya Mpanda  Coronel Bruno amesema kuwa  ongezeko la Ugonjwa huo inatokana na Wananchi kutokuzingatia  kupima Afya kila mara ili kubaini.” Picha na Mtandao. Na Veronica Mabwile-katavi Baadhi ya Wananchi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi  wameiomba Serikali mkoani…

7 March 2024, 2:53 pm

Mpanda, Watoto Yatima na Mazingira Maalumu Waguswa na Msaada

“Matendo hayo ya huruma yamefanyika katika shule ya Msingi Nyerere na katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Yohana Paul wa pili Matumaini ya Watoto ambapo wamegawa mahitaji kama vile Madaftari , Mchele, na Juice” Picha na Lillian Vicent“ Na…

7 March 2024, 2:31 pm

MPANDA, Madiwani Wahofia Bajeti Ya TARURA

“Madiwani Wa Halmashauri ya Manispaa Ya Mpanda Wameonyesha Kutoridhishwa Na Bajeti Hiyo Na Kumtaka Manager Wa Tarura Kwenda Kupitia Upya Na Kuiwasilisha Kwa Baraza Hilo Ifikapo Jumatatu ya tarehe 11 mwezi wa tatu mwaka huu” Picha na Deus Daud Na…

7 March 2024, 1:55 pm

KATAVI, Aliebaka Afariki Akipatiwa Matibabu

“Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema mtuhumiwa alifikishwa mikononi mwa Jeshi hilo akiwa na hali mbaya hivyo muda mchache baada ya kufikishwa hospitali alifariki dunia na mwili kukabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya mazishi” Picha na…

5 March 2024, 3:13 pm

Mfungwa atuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 13 Katavi

“Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema suala hilo lipo katika uchunguzi na hatua kali za kisheria zitachukuliwa huku wao kama serikali wamesikitishwa kutokea kwa tukio hilo” Na Gladness Richard-Katavi Binti mwenye umri wa miaka 13 mkazi wa kijiji…

20 February 2024, 5:24 pm

Wabeba taka Mpanda wameshindwa kazi?

Wananchi wamesema mtaa huo umekuwa na harufu kali ambayo imekuwa haivumiliki na wamekosa namna  ya kufanya hivyo wanahifadhi kwenye mifuko  kwa sababu taarifa za taka hizo wamelalamika kwa viongozi wao bila mafanikio yeyote. Na Samwel Mbugi-Katavi Wananchi wa kata ya…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.