Mpanda FM

Recent posts

28 March 2024, 1:18 pm

Waliochomewa tumbaku Mpanda kutafutiwa ufumbuzi

“Katika uvamizi huo jumla ya majengo kumi ya kukaushia Tumbaku yamechomwa moto pamoja na stoo mbili pamoja na wananchi hao kuchukuliwa mali zao ikiwemo simu za mkononi pamoja na fedha.” Picha na Betord chove Na Bertod Chove-katavi Serikali wilayani Mpanda…

26 March 2024, 12:42 pm

Walimu wakuu watoroka chama Katavi

“Ikiwa  ni mara ya kwanza kwa  mkutano mkuu wa walimu wakuu wa shule za msingi mkoa wa Katavi uliofanyika katika ukumbi wa manispaa huku ukiambatana na mafunzo ya uongozi na taaluma,huku ikiambatana na kauli mbiu isemayo ‘‘Tekeleza Mikakati Boresha Elimu…

22 March 2024, 2:24 pm

Zaidi ya Vitambulisho Elfu 64 vya NIDA Vyaletwa Mpanda

“Wananchi amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kwani vimewaondoa hofu ya kukosa huduma muhimu ambazo zinaambatana na vitambulisho vya taifa kama vile kufungua akaunti za Benk“ Picha na Samweli Mbugi Na Samweli Mbugi-katavi Wananchi wa kata ya Mwamkulu Wilaya ya Mpanda mkoani…

21 March 2024, 10:55 am

Wananchi Katavi hawana elimu ya utunzaji wa kinywa, meno

Picha na Mtandao “Utafiti uliofanyika umegundua kuwa watoto  wenye umri wa miaka sita hadi tisa ndio waathirika wakubwa“ Na Samwel Mbugi -Katavi Wananchi Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni  mseto kuhusiana na maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa…

21 March 2024, 9:32 am

Umaskini watajwa chanzo cha ukatili wa kijinsia kwa wanawake Katavi

 “Jamii inapaswa kupewa elimu juu ya namna ya kumwinua mwanamke kiuchumi pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuwepo na usawa wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke“ Na Rachel Ezekia-Katavi Umaskini umetajwa kuwa chanzo cha ukatili wa kijinsia kwa…

20 March 2024, 4:02 pm

Mpanda, Vibaka Waibuka Mpanda Girls

“Mwenyekiti wa mtaa wa Mtemi Beda Edisi Kazwika amekiri kupokea tarifa za uwepo wa matukio ya uhalifu katika eneo hilo na kuwahakikishia hatua za usalama zinachukuliwa kwa wananchi wanaopita katika eneo hilo” Picha na mtandao Na Rachel Ezekia-katavi Wananchi wa…

19 March 2024, 3:19 pm

Katavi, Wafanyabiashara 24 Mbaroni Kupandisha bei ya Sukari

Picha na Mtandao “Ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuzingatia bei  elekezi inayotolewa na Serikali ili kupunguza usumbufu kwa mlaji“ Na Betord Benjamin-Katavi Jumla ya Wafanyabiashara 24 Katika Manispaa ya Mpanda Mkoani  Katavi wamekamatwa kutokana na kuuza sukari kinyume na bei…

18 March 2024, 2:08 pm

Waliofyekewa mahindi Katavi washukuru mchango wa Mpanda Radio FM

“Wakulima hao walifyekewa mahindi baada ya kile kilichosemwa ni ukiukwaji wa sheria ya kulima mazao marefu kwa Manispaa ya Mpanda katika maeneo yaliyokatazwa, lakini yaliacha maswali baada ya kadhia hiyo kuwakumba wakulima watatu pekee huku maeneo mengine mazao yakiendelea kuachwa“…

15 March 2024, 6:01 pm

KATAVI, TMDA Yabaini Ongezeko la Ugonjwa wa Figo

“Kuna changamoto ya Ini na Figo kushindwa kufanya kazi, na Saratani kuongezeka katika Jamii Yanayosababishwa na  matumizi mabaya ya dawa kwa baadhi ya Wananchi” Picha na Mtandao Na Samwel Mbugi-katavi Mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA] kutoka makao Makuu…

Kuhusu Mpanda Radio

Umiliki wa redio
Mpanda Radio FM inamilikiwa na kampuni iliyosajiliwa iitwayo Mpanda radio FM Limited na cheti cha usajili namba 78298 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpanda Radio FM pia imesajiliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania TCRA, Wizara ya Viwanda na biashara; ama tunatambuliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA na Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kama Mlipa Ushuru, tuna Namba ya Kitambulisho cha Mlipa kodi 115-577-239 na tumepewa nambari ya usajili ya VAT 40-015708 kwa Biashara iliyoko hoteli ya Mpanda, eneo la eneo. nambari G, nambari ya kuzuia 35.

Dira
Kuwa jamii thabiti yenye afya bora, elimu, umoja na maendeleo endelevu, inayotambua wajibu na haki.

Dhamira
Kushirikisha jamii katika kuandaa vipindi, habari na uendeshaji wa redio kwa kuzingatia taaluma. Kuwa jukwaa la mijadala inayochochea mabadiliko chanya ya fikra, usawa wa jinsia, sheria na utawala bora, uwajibikaji, ushindani wa maendeleo, utamaduni na ulinzi wa rasilimali.

Uongozi
Mpanda Radio FM ina mlolongo mzuri wa uongozi na inasimamiwa na Bodi ya wakurugenzi. Tuna wakurugenzi watatu kwa hisa na kuajiriwa; pia tuna uongozi wa uzalishaji na uuzaji.