Katavi walaumu wanaoficha vitendo vya ukatili wa kijinsia
18 September 2024, 12:03 pm
“Vitendo vya ukatili wa kijinsia havifai na vinapaswa kukemewa kwani vinazidi kukithiri na kuleta athari kubwa haswa kwa watoto na wanawake.“
Na Lazaro Maduhu-Katavi
Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali iweke juhudi ya ufutiliaji wa masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwemo vitendo vya ulawiti na ubakaji.
Wameyasema hayo walipokuwa wakizungumza na Mpanda radio FM huku wakibainisha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia havifai na vinapaswa kukemewa kwani vinazidi kukithiri na kuleta athari kubwa haswa kwa watoto na wanawake.
Wananchi hao wamesema kuna haja wao kama wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua vitendo hivyo na kuacha kuficha uovu huo.
Sauti ya wananchi wakizungumza
Hivi karibuni kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Gogfrey Eliakim Mnzava akifungua klabu ya kupambana na kuzuia madawa ya kulevya na ukatili wa kijinsia katika shule ya sekondari Magamba amekemea vitendo hivyo na kuiomba serikali mkoani katavi kuunga mkono klabu hiyo katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Sauti ya kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Gogfrey Eliakim Mnzava
Vitendo vya ukatili wa kijinjisa vimekuwa vikijitokeza katika jamii ambapo baadhi ya familia hawataki kuyaweka wazi matendo hayo maovu jambo ambalo linachangia ongezeko la matendo ya namna hiyo kwa wananchi.