Wakuu wa idara Tanganyika watakiwa kujibu hoja zinazoibuliwa na CAG
2 July 2024, 11:13 am
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bw. Charles E. Kichere
“Wakuu wa idara na vitengo wenye tabia ya kutoshiriki kujibu hoja zinazoibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni kitendo ambacho kinaibua maswali“
Betord Chove -Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kuwasimamia wakuu wa idara na vitengo wenye tabia ya kutoshiriki kujibu hoja zinazoibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kitendo ambacho kinaibua maswali.
Mrindoko ametoa maagizo hayo Juni 29, 2024 kupitia Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi Albert Msovela aliyemwakilisha katika mkutano wa Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Tanganyika wa kupitia na kujadili hoja za Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tanganyika Shaban Juma ameahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizoibuliwa kwa kuunda timu ya utekelezaji.
Ikumbukwe ushauri huo umetolewa na CAG. Chambi Sasamka ili kuongeza uwajibikaji katika halmashauri hiyo licha ya kupata hati inayoridhisha.