Mabomu ya jeshi la polisi yawa kero kwa wananchi mkoani Katavi
15 May 2024, 11:04 am
Picha na Gladness Richard
“zoezi la kusikiliza kero za wananchi ni kwa kila kata ambapo jeshi la polisi litahakikisha linawafikia wananchi wote katika kata hizo“
Na Samwel Mbugi -Katavi
Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani ameanzisha ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kila kata ndani ya mkoa wa Katavi.
Wakieleza kero katika mkutano uliofanyika manispaa ya Mpanda wananchi wameainisha kero ya mabomu wakati wa mazoezi ya jeshi la polisi mkoa wa Katavi ambayo yameonekana kuwakosesha utulivu wananchi kufanya shughuli za maendeleo kero kwa wanaoishi karibu na maeneo wanayofanyia mazoezi
Sauti ya Wananchi mkoa wa katavi wakieleza kero zao
Kamanda wa polisi amethibitisha kuwa ni kweli kunawakati wanaripua mabomu wakati wa mazoezi yao na amewaomba radhi wananchi wanaishi karibu na eneo la jeshi la polis
Sauti ya kamanda wa jeshi la Polisi Kaster Ngonyani akijibia kero hizo
Hata hivyo kamanda Ngonyani amesema kuwa zoezi hili la kusikiliza kero litakuwa endelevu ambapo atahakikisha anapita kila kata kujua kero za wananchi wa eneo husika.