Mpanda FM
Mpanda FM
2 April 2026, 6:14 pm

“Elimu utolewe kwa wanawake kuhusu umuhimu wa mavazi ya heshima”
Na Anna Mhina
Baadhi ya wanaume manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameomba serikali kusisitiza maadili kwa wanawake juu ya umuhimu wa uvaaji wa mavazi ya maadili ili kuepukana na vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wanaume hao wamesema kuwa kumekuwa na ongezeko la wanawake kuvaa mavazi yasiyo na heshima ambayo huchangia kuchochea vitendo hivyo vya kikatili.
Kwa upande wao baadhi ya wanawake wameeleza sababu zinazopelekea kuvaa mavazi yasio na maadili ikiwa ni pamoja na kutaka kuendana na kasi ya utandawazi huku wengine wakisema ukosefu wa elimu ya maadili, kutojitambua na kujithamini.
Anyulumye Longo ni afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda amewasihi wanawake kuacha kuvaa mavazi yasiyo na maadili kwani yanashawishi vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji.