Mpanda FM
Mpanda FM
1 April 2026, 9:19 am

“Uzalendo unaleta amani na kudumisha utamaduni”
Na Leah Kamala
Wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa maoni yao kuhusiana na umuhimu wa kijana kuwa mzalendo, huku wakisisitiza kuwa uzalendo ni msingi wa maendeleo ya taifa.
Wakizungumza na mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa vijana wanapaswa kuipenda nchi yao kwa vitendo na kuilinda amani ya nchi yao.
Kwa upande wake afisa maendeleo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Michael Mikingi amesema kuwa uzalendo unachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla huku akiwataka vijana kuwa tayari kulinda amani na kuunga mkono juhudi za serikali.