Mpanda FM

Kupanda kwa bei ya nyama, kilio kwa wafanyabiashara

26 March 2026, 6:11 pm

Picha na John Benjamin

“Biashara imekuwa ngumu”

Na John Benjamin

Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia kupanda kiholela bei ya nyama ya ng’ombe kutoka shilingi 10,000 hadi shilingi 12,000.

Wakizungumza na Mpanda Redio FM kwa nyakati tofauti  wamesema kuwa kupanda kwa bei ya kitowewo hicho imewafanya kushindwa kumudu gharama na kuiomba serikali kuingilia kati swala hilo ili kuhakikisha bei inashuka na kuendana na hali ya maisha ya wananchi wa kawaida.

Sauti za wananchi

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wa bucha za nyama manispaa ya Mpanda wamesema kuwa kasi ya wanunuzi imepungua ukilinganisha na awali ambapo  ameleeza kuwa hali hiyo imekuwa ikiwagharimu  ambapo imekuwa ikisababisha kukaa kwa muda mrefu buchani.

Sauti za wafanyabiashara

Mwenyekiti wachinjaji mkoa wa Katavi Fadhili Makolokolo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ambapo amesema kuwa kupanda kwa bei ya nyama imesababishwa na kupanda kwa bei ya mifugo haswa Ngombe na hilo limesababishwa na uwepo wa wimbi la wanunuzi kutoka nje ya nchi.

Sauti za wachinjaji

Aidha Makolokolo ameiomba serikali kusimamia vyema wanunuzi wanaotoka nje ya nchi kuhakikisha wanafata sheria pindi wanapoingia nchi kununua mifugo.