Mpanda FM

Kisaka” Msitumie maji ya mtoni”

26 March 2026, 5:42 pm

Moja ya mto uliopo Mpanda. Picha na Leah Kamala

Ni vema wananchi wawe na desturi ya kuchemsha maji ili kuepukana na magonjwa”

Na Roda Elias

Jamii iishiyo karibu na vyanzo vya maji hususani mito  katika manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imetakiwa  kuacha matumizi ya maji yasiyo safi na salama ili kulinda afya zao.

Hayo yamesemwa na afisa afya wa manispaa ya Mpanda Erick Kisaka kutokana na baadhi ya wananchi hao kuwa na mazoea ya kutumia maji yanayopatikana katika mto uliopo kando kando na makazi yao

Akizungumza na mpanda radio FM afisa afya huyo amesema kuwa maji ya mto sio safi na salama kwani yana mchanganyiko wa vitu vingi vichafu na kwa kutumia maji hayo ndio chanzo ya magonjwa ya mripuko.

Aidha Kisaka  ametoa wito kwa jamii kuwa na desturi ya kuchemsha maji na kuweka vidonge vya kutibu maji ili kuepukana na magonjwa.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kuwa mazoea na kukwepa gharama ya maji ya bomba inawalazimu kutumia maji ya mto huo kwa matumizi ya nyumbani kama kuosha vyombo na matumizi mengine.