Mpanda FM

Waganga tiba asili Katavi wajitokeza kwa wahitaji

20 March 2026, 5:55 pm

Mwenyekiti wa tiba asili mkoa wa Katavi aliyevaa suti ya bluu akiwa ameambatana na waganga wengine na kumtembelea mama anayeuguza mtoto aliyevaa gauni la bluu la maua.picha na Aidan

“Ni vyema kurudisha shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa kuyafanya matendo hayo ya huruma “

Na Anna Milanzi- Katavi

Waganga wa tiba  asili na tiba mbadala mkoa wa Katavi wamefanya matendo ya huruma kwa kuwatembelea watoto yatima na mama mjane anayeuguza mtoto wake.

Akizungumza kwa niaba ya waganga wa tiba asili Mwenyekiti wa tiba asili na tiba mbadala mkoa wa Katavi Gadius Luviga amesema wameona ni vyema kurudisha shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa kuyafanya matendo hayo ya huruma .

Sauti ya mwenyekiti wa tiba asili na tiba mbadala mkoa wa Katavi Gadius Luviga

Akitoa shukrani mara baada ya kupatiwa kiasi cha fedha cha Tshs laki moja mama anayeuguza mtoto mkazi wa mtaa wa Mpanda hotel amesema kiasi hicho cha fedha kimesaidia kupunguza kiasi cha fedha kinachohitajika katika matibabu ya mtoto wake.

Sauti ya Mama anayeuguza mtoto

Aidha  wametembelea katika  kituo cha kulelea watoto cha Yohana Paulo wa pili kilichopo manispaa ya Mpanda ambapo afisa ustawi mlezi wa kituo hicho ameeleza  kuwa wamekuwa wakiwalea watoto waliopoteza wazazi wote wawili na hawana msaada,watoto waliotelekezwa,watoto ambao wazazi wao wanachangamoto ya afya ya akili pamoja na watoto wanaopitia ukatili .

Sauti ya afisa ustawi mlezi wa kituo hicho.

Waganga wa tiba asili mkoa wa Katavi walipotembelea katika kituo hicho cha kulelea watoto yatima wametoa kiasi cha Tshs laki mbili fedha ambayo itasaidia katika mahitaji ya watoto na kuwaomba watu wengine kuendelea kuwatembelea watoto hao