Mpanda FM
Mpanda FM
11 March 2026, 4:58 pm

“Kila taasisi ipande miti”
Na Leah Kamala
Wananchi manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameelezea kero mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao, na kumuomba mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko kuzifanyia kazi ili kuboresha maisha yao.
Kero hizo ziliwasilishwa na wananchi katika kliniki ya kusikiliza kero, iliyohudhuria na mkuu wa mkoa wa Katavi, pamoja na viongozi wengine na mkoa, katika ukumbi wa manispaa.
Akizungumza wakati wa kusikiliza na kupokea kero mbalimbali za wananchi, mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa changamoto zinazowakumba wananchi zinaendelea kupatiwa ufumbuzi, huku akisisitiza kufanya usafi ndani ya saa72, pamoja na upandaji wa miti ili kuimarisha afya ya wananchi
Viongozi wa mkoa wa Katavi wamewahakikishia wananchi kuwa serikali itaendelea kusikiliza na kutatua changamoto zao, na kuboresha huduma za kijamii