Mpanda FM
Mpanda FM
5 March 2026, 1:47 pm

“Watoto wetu wanateseka”
Na Anna Mhina
Wananchi wa kitongoji cha Mbogwe kilichopo kijiji na kata ya Kabungu wilayani Tanganyika mkoani Katavi wameiomba serikali kuingilia kati ujenzi wa shule ya msingi ulioanzishwa katika kitongoji hicho.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa baadhi ya watoto wamelazimika kukatisha masomo kutokana na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa wakiwa njiani hali iliyopelekea wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa kijiji kuanza mchakato wa kujenga shule.
Akizungumza kwa niaba ya serikali ya kijiji mwenyekiti wa kitongoji cha Mbogwe David Richard Mbogo amekiri kuwepo kwa mpango huo wa ujenzi wa shule ya msingi na kuwatoa hofu wananchi kuwa kwa sasa wanasubiri ramani ili kuendelea na kazi.
Hata hivyo mpaka sasa wananchi wa kitongoji cha Mbogwe wamefanikiwa kununua kiwanja chenye ukubwa wa zaidi ya ekari tano na matofali elfu 5 pamoja na pesa kiasi cha shilingi million 3 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa msingi.