Mpanda FM
Mpanda FM
26 February 2026, 3:06 pm

Mhandisi Philipo Pagati meneja usambaji maji manispaa ya Mpanda. Picha na Anna Mhina
“Kwa kweli kuna changamoto kubwa ya maji”
Na Leah Kamala
Wananchi kata ya makanyagio manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia upatikanaji wa maji safi na salama hali inayowalazimu kutumia maji kutoka vyanzo vya maji visivyo salama.
Wakizungumza na Mpanda radio fm, wananchi hao wamesema kuwa kumekuwa na idadi ndogo ya siku za upatikanaji maji ambayo hayatoshelezi kwa familia zao
Akijibu malalamiko hayo kaimu mkurugenzi mtendaji ambaye pia ni meneja usambaji maji manispaa ya Mpanda Mhandisi Philipo Pagati amesema kuwa Idara inaendelea na jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kupitia mpango mkakati utanaotekelezwa wa mradi wa maji wa miji 28 unaotarajia kukamilika Julai mwaka huu.
Nae afisa afya manispaa ya Mpanda Ibrahim Mikidai amewataka wananchi kutibu maji wanayotumia ambayo hawana uhakika na yanapotoka pamoja na yale ya visimia ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu