Mpanda FM
Mpanda FM
18 February 2026, 9:00 am

“Wamepongeza hatua hiyo ya kuboresha miundombinu ya ofisi na kuwataka wadau wengine kujitokeza ili kuendelea kuboresha miundombinu ya ofisi”
Na Betord Chove-Katavi
Wananchama wa jumuiya mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kujitoa ili kuboresha Miundombinu ya Chama cha Mapinduzi .
Wito huo umetolewa na Geofrey Alfonce Kipeta ambaye ni Afisa Tehama wa wilaya wa chama cha mapinduzi {CCM} mara baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ukarabati ofisi ya jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi{UVCCM} wilaya ya Mpanda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mpanda joseph Ngoma na katibu wa jumuiya hiyo wamepongeza hatua hiyo ya kuboresha miundombinu ya ofisi na kuwataka wadau wengine kujitokeza ili kuendelea kuboresha miundombinu ya ofisi.
Vifaa vya zaidi ya shilingi laki nane vimekabidhiwa kwa ajili ya ukarabati wa ofisi ya UVCCM wilaya ya Mpanda ambapo baadhi ni mbao, sement, mabati, huku ahadi ikitolewa kwa ajili ya kusimamia gharama zote za ukarabati mpaka utakapokamilika.