Mpanda FM

Rungu zito kwa watumiaji wa madawa ya kulevya

6 February 2026, 5:07 pm

Christina Ruchahura kamisha wa mamlaka ya udhibiti na kupambana na madawa ya kulevya  Kanda ya magharibi. Picha na Samwel Mbugi

“Hii mamlaka imeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya kudhibiti na kupambana madawa ya kulevya”

Na Samwel Mbugi

Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuendelea kutoa taarifa ya uwepo wa  matumizi ya madawa ya kulevya katika maeneo wanayoishi, jambo ambalo litasaidia kupata nguvu kazi ya vijana kwa taifa.

Hayo yamebainishwa na ofisa wa mamlaka ya udhibiti na kupambana na madawa ya kulevya Dezidel Tumbu ambapo amesema mkoa wa Katavi ni miongoni wa mikoa ambao unakabiliwa na baadhi ya wananchi kujishugulisha na kilimo na matumizi ya  bangi Kwa asilimia kubwa licha ya kuwa ni kinyume cha Sheria.

Sauti ya Tumbu

Dezidel Tumbu ofisa mamlaka ya udhibiti na kupambana na madawa ya kulevya.

Kwa upande kamisha wa mamlaka ya udhibiti na kupambana na madawa ya kulevya  Kanda ya magharibi Christina Ruchahura amesema kuwa zipo sheria zilizotungwa na bunge la jamuhuri ya Tanzania  ambazo zinawajibisha watumiaji,wauzaji na wanaofanya kilimo cha madawa ya kulevya.

Sauti ya Christina

Serikali nchini Tanzania kupitia Kwa mamlaka ya udhibiti na kupambana na madawa ya kulevya inaendelea kufanya jitihada mbali mbali na tasisi zingine kama vile Takukuru ili kuhakikisha wanatokomeza wimbi la matumizi ya madawa ya kulevya nchini Tanzania