Mpanda FM

Mpanda wachoshwa na madereva wasioheshimu vivuko vya watembea kwa miguu

5 February 2026, 4:40 pm

Coplo Sophia Peleka askari kitengo cha elimu ya usalama barabarani Katavi. Picha na Anna Mhina

“Madereva hilo hawalizingatii sana kwa mkoa wetu”

Na Anna Mhina

Baadhi ya watembea kwa mguu manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamewalalamikia badhi madereva wa vyombo vya moto kutotii sheria za usalama barabarani.

Wakizungumza na Mpanda redio FM wamesema kero kubwa wanayoipata barabarani ni maeneo ya vivuko vya watembea kwa mguu ambapo madereva wengi hawazingatii sheria za vivuko hivyo hali inayopelekea kuhatarisha usalama wao.

Sauti za wananchi

Wakijibu malalamiko hayo baadhi ya madereva wa vyombo vya moto wamesema kuwa ukosefu wa elimu ya matumizi ya barabara ndio chanzo huku wengine wakihitaji elimu itolewe kwa wanafunzi wamekuwa wakicheza kwenye vivuko hivyo.

Sauti za madereva

Kwa upande wake Coplo Sophia Peleka ambaye ni askari wa jeshi la polisi Tanzania anayefanya kazi kitengo cha elimu ya usalama barabarani mkoa wa Katavi amewataka madereva kutii sheria za usalama barabarani.

Sauti ya Coplo Sophia