Mpanda FM

Serikali ya mtaa wa Mpanda hotel yajipanga kutengeneza madawati

14 January 2026, 5:47 am

Madawati mabovu yaliyopo katika shule ya msingi Mpanda. Picha na Rhoda Elias

“Tayari tumeshawaelekeza mafundi wamekuja na kufanya tathimini yao”

Na Rhoda Elias

Serikali ya mtaa wa Mpanda hotel imefanya ziara  katika shule ya msingi Mpanda  iliyopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi na kuchukua hatua ya kutengeneza madawati mabovu katika shule hiyo.

Akiwa katika ziara hiyo iliyofanyika January 13, 2026 mwenyekiti wa mtaa wa Mpanda hotel Ibrahim Ally Msanda amesema kuwa tayari wametoa tenda kwa mafundi ili kutengeneza madawati hayo na kwamba kazi hiyo ya utengenezaji inapaswa kuanza .

Sauti ya mwenyekiti

Akisoma taarifa ya shule mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi Mpanda Stephano Mwalisu ameinisha changamoto ya utoro kwa baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo.

Sauti ya mwalimu mkuu msaidizi

Akijibia taarifa hiyo mwenyekiti Msanda amesema kuwa wataanza msako kuanzia kwa wazazi ambao hawafuatilii watoto kwenda shule.

Sauti ya mwenyekiti