Mpanda FM

Mkombozi Paralegal watoa elimu ya ukatili Katavi

10 January 2026, 3:41 pm

Afisa maendeleo akitoa elimu kwa wananchi. Picha na Anna Milanzi

“Tunawajengea uwezo kamati hizo kwa kuziimarisha”

Na Anna Milanzi

Taasisi ya Mkombozi Paralegal iliyopo mkoani Katavi imeendelea kuwawezesha wananchi kupata elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia na kuwawezesha kutambua sehemu za kuripoti matukio hayo.

Afisa tathimini na ufuatiliaji kutoka taasisi ya  mkombozi paralegal, George Kasambwe amesema elimu hiyo inatolewa kutokana na mradi wa sauti ya mwanamke ambao umelenga kuziwezesha kamati zinazopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ngazi ya mtaa na kata.

Sauti ya Kasambwe

Respista Kalugendo afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda ambaye pia ni mratibu wa kamati za MTAKUWWA Halmasauri ya manispaa ya Mpanda amesema kamati zimewezeshwa mambo mbalimbali na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kamati hizo.

Sauti ya afisa maendeleo

Wajumbe wa kamati hizo wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi wamesema mafunzo hayo yamekuwa ni msaada mkubwa kwao na watakwenda kutoa elimu kwa wananchi wengine pamoja na wanafunzi kutoa elimu hiyo waliyoipata   shuleni kwao.

Sauti ya wajumbe

Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku nne kupitia taasisi ya  mkombozi paralegal inayojihusisha na usaidizi wa masuala ya kisheria mkoa wa katavi huku mradi huo ukiwa umefadhiliwa na  taasisi ya Inabel.