Mpanda FM
Mpanda FM
26 November 2025, 10:30 am

“Hakikisheni mnakuwa wabunifu katika kutoa huduma”
Na Restuta Nyondo
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ameziagiza taasisi zote za umma kutoa huduma bora na ufanisi kwa wananchi na kuhakikisha wanakua wabunifu katika utoaji wa huduma bila visingizio.
Ameyasema hayo katika kikao cha wakuu wa taasisi mkoa wa Katavi ambapo amesema kuwa taasisi za umma ni moyo wa serikali na hivyo ni muhimu kuwajibika katika kutatua changamoto za wananchi.
Mpanda radio FM imezungumza na baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda ambapo wamedai kuwa bado baadhi ya maeneo ya kutolea huduma ikiwemo huduma za afya kuna changamoto ya kupata huduma kwa wakati.
Hayo yanajiri wakati serikali mkoani Katavi ikiwa imetoa siku tatu kuanzia Novemba 25 kwa wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero ili kutatua changamoto hizo kutokana kuwepo kwa malalamiko mbalimbali.