Mpanda FM
Mpanda FM
25 November 2025, 7:01 pm

“Sisi tunathamini mchango mnapokuwa na jambo lolote mtufikie”
Na John Benjamin
Wananchi wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wameaswa kudumisha amani na mshikamano utakaokuwa nyenzo muhimu wa kufanya shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa masirahi taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumza ofisini kwake na kamati ya Amani na Maridhiano ya wilaya, viongozi wa dini mbalimbali na viongozi wa vyama vya siasa amesisitiza msingi wa maendeleo ni amani.
Aidha Jamila amesema serikali ipo kwenye mpango wa kuwatabua vijana waliomaliza kidato cha nne, sita na vyuo vikuu ili kuwawezesha kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo wilayani humo ili kuwainua kiuchumi.
Nao baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamesema,kupitia nafasi zao katika jamii, wataendelea kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda amani na kuimarisha mshikamano ili kuifanya Mpanda sehemu salama ya maendeleo
Wajumbe wa kamati hiyo ya amani na maridhiano wamesisitiza kuwa majadiliano yaliyofanyika yameonyesha dhamira ya pamoja ambayo inaimarisha umoja na mshikamano.