Mpanda FM
Mpanda FM
20 November 2025, 11:58 am

“Ofisi ya makamu wa raisi na waziri mkuu ziunganishe mfuko wa maafa”
Na Restuta Nyondo
Tanzania imepata nafasi ya kipekee ya kunufaika na ruzuku ya dola za Marekani milioni 20 (takriban Sh. bilioni 48), kutoka Mfuko wa kukabiliana na Hasara na Uharibifu (FRLD), ulioundwa kusaidia nchi zinazokumbwa na mabadiliko ya tabianchi.
Juma Maziku kutoka shirika la Ujerumani GIZ linalotekeleza mradi wa IKI KATUMA mkoa wa Katavi amefanya mazungumzo na Mpanda redio fm ambapo amesema ili fedha ziwafikie wananchi katika kukabiliana na changamoto hiyo ni lazima uwekwe mkakati shirikishi kwa jamii katika kushughulikia hasara na uharibifu katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.