Mpanda FM
Mpanda FM
18 November 2025, 6:16 pm

Viongozi wa bodaboda Katavi wakiwa kwenye picha ya pamoja na bodaboda. Picha na Samwel Mbugi
“Lengo ni kuwapongeza bodaboda wa Katavi kwa kuendelea kuitunza amani”
Na Samwel Mbugi
Mwenyekiti wa umoja wa maafisa usafirishaji (Bodaboda) mkoa wa Katavi Isack Daniel Joseph ameahidi kuendelea kuitunza amani na utulivu kipindi chote kama serikali inavyosisitiza
Akizungumza na wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ofisini kwake Isack amewapongeza bodaboda wa kanda zote za mkoa wa katavi kwa kuhakikisha wanaendelea kuwa watulivu na kuitunza amani iliyopo
Pia amewataka viongozi wote wa kanda zote za mkoa wa Katavi kuhakikisha wanawapokea bodaboda walio na vielelezo kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa pamoja na vitambulisho vinavyoonyesha kuwa ni mkazi wa maeneo husika.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa kanda mbalimbali za mkoa wa katavi wametoa shukurani kwa viongozi wao wa ngazi ya mkoa kwa kuendelea kuwasimamia vyema na kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kuwepo.
Hata hivyo wametoa shukurani kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuanzisha wizara ya vijana ambayo itaenda kushughulikia changamoto zote zinazowahusu vijana.