Mpanda FM

Wagonjwa Katavi wanufaika na simba day

11 September 2025, 12:22 pm

Mashabiki wa simba wakitoa zawadi kwa uongozi wa kituo cha afya Itenka. Picha na Anna Mhina

“Tunawashukuru sana wanasimba kwa kutukumbuka”

Na Anna Mhina

Jamii imeshauriwa kujitokeza katika kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu katika vituo vya afya ili kuweza kuokoa maisha ya binadamu.

Hayo yamesemwa na mtendaji kata ya Itenka Yegela Samike alipokuwa akikabidhi zawadi zilizotolewa na mashabiki wa klabu ya Simba tawi la Itenka kwa uongozi wa kituo cha afya cha kata hiyo.

Sauti ya mtendaji

Akipokea zawadi hizo dokta James Kisoo ambaye ni afisa muuguzi msaidizi wa kituo cha afya cha Itenka ameushukuru uongozi wa mashabiki wa klabu ya simba kwa kuona umuhimu wa kuwakumbuka wagonjwa kwa kuwapa zawadi.

Sauti ya doctor

Kwa upande wao baadhi ya wanufaika ambao ni wagonjwa katika kituo hicho cha afya wamefurahi kupokea zawadi hizo na kuwaomba waendelee na moyo huohuo.

Sauti ya wagonjwa

Licha ya zawadi mbalimbali zilizotolewa na mashabiki wa klabu hiyo ya simba pia wamefanikiwa kuchangia damu katika kituo hicho cha afya cha Itenka.