Mpanda FM
Mpanda FM
1 September 2025, 7:49 pm

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko. Picha na Restuta Nyondo
“Niwasihi wanakatavi jitokezeni kushiriki mikutano ya kampeni”
Na Restuta Nyondo
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wananchi kuepukana na vitendo vya uvunjifu wa sheria na vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika kipindi cha kampeni na uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mrindoko amesema kuwa jukumu la kutunza amani na usalama ni la kila mwananchi huku akiwataka viongozi kuanzia ngati ya mitaa kuimarisha usalama katika maeneno yao.
Mrindoko amesema kuwa serikali na vyombo vyote vya usalama mkoani hapa vimejipanga kuhakikisha kuwa hatua zote za kuelekea uchaguzi zinafanyika na kuzingatia ushiriki wa makundi yote.
Katika hatua nyingine amewataka wananchi waliojiandikisha kutunza vitambulisho vyao vya kupigia kura ili waweze haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka.
Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na raisi ifikapo October 29, 2025.