Mpanda FM
Mpanda FM
30 August 2025, 1:10 pm

“Hatuna utaratibu wa kuwakata wagonjwa wetu miguu”
Na Anna Mhina
Baadhi ya madereva pikipiki maarufu kama bodaboda wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuingilia kati suala la kupatiwa haki ya huduma za kiafya pindi wanapopata ajali.
Wakizungumza na Mpanda radio FM madereva hao wamewalalamikia baadhi ya wahudumu wa afya kutotenda haki kwa kutowajali ikiwa ni pamoja na kutowapa huduma zinazostahili.
Akijibu malalamiko hayo mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Katavi ambaye ni daktari bingwa mbobezi upasuaji wa mifupa Deogratias Banuba amesema wanatoa huduma sahihi kwa kila mgonjwa na kukanusha taarifa ya ukatwaji wa miguu kiholela kwa madereva bodaboda .
Hivi karibuni kumekuwa na uvumi miongoni mwa waendesha bodaboda kudai kuwa pindi wanapopata ajali hukatwa miguu na kutokupewa huduma stahiki wanapofika katika vituo vya afya.