Mpanda FM

SP Sukunala “dereva bajaji lazima uwe na leseni”

4 August 2025, 3:24 pm

Mkuu wa usalama barabarani SP. Sukunala Katavi akitoa maelekezo kwa madereva bajaji. Picha na Samwel Mbugi

“Lazima tukemee ajali na tujitahidi kuwa naleseni za udereva”

Na Leah Kamala

Mkuu wa usalama barabarani manispaa ya mpanda mkoani katavi, SP. Efeso Sukunala amesema kuwa ni lazima kila dereva kuwa na leseni ili kuepuka na changamoto anazoweza kukumbana nazo awapo barabarani.

Ameyasema hayo katika kikao na maafisa usafirishaji maarufu kama bajaji kilichofanyika katika ukumbi wa polisi club manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.

Sauti ya Sukunala

Aidha Sukunala amewasihi maafisa usafirishaji kutozidisha abiria ili kufuata sheria za barabarani  hivyo kusafirisha abiria wasiozidi watatu na wa kwanza akiwa ni dereva ndani ya bajaji.

Sauti ya Sukunala

Nae kiongozi wa nidhamu manispaa ya Mpanda Mrisho Seleman Ally amesema kuwa kanuni na vituo vyote vimezingatia  sheria na kanuni za jamhuri ya muungano wa Tanzania, hivyo ni vyema kutii sheria ilizowekwa na mamlaka

Sauti ya kiongozi wa nidhamu

Akihitimisha kikao hicho nae mwenyekiti wa madereva bajaji ametoa maagiza kwa wenyeviti wa vituo kufikisha taarifa za vikao kwa wanavituo wote kwa ajili ya kujenga amani na kupunguza ajali.