Mpanda FM
Mpanda FM
30 July 2025, 9:29 am

Mkuu wa mkoa wa Katavi akizungumza na madereva bajaji. Picha na Samwel Mbugi
“Kuna mambo bado hayajakaa sawa niwape muda mkayatafakari upya”
Na Samwel Mbugi
Baadhi ya madereva bajaji mkoa wa Katavi wamelalamika kwa mkuu wa mkoa kuhusu kuamriwa kushusha abiria nje ya stendi kuu Mizengo Pinda pamoja na tozo wanazotoa.
Hayo yamejiri wakati mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko alipofika kusikiliza kero ambazo wanakumbana nazo abiria pamoja na wananchi wanaofanya shughuli ndani ya stendi
Kupitia changamoto hizo mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amemuagiza mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda pamoja na viongozi wa stendi hiyo ndani ya mwezi mmoja wawe wametatua changamoto hiyo ambayo inawakumba madereva bajaji.
Hata hivyo Mrindoko ameuagiza uongozi wa manispaa ya Mpanda kuhakikisha usafi unadhibitiwa kikamilifu ndani na nje ya stendi ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.