Mpanda FM

Madereva, makondakta Katavi wapewa onyo

18 July 2025, 11:50 am

Baadhi ya madereva na makondakta wa stendi ya zamani. Picha na Leah Kamala

“Ni marufuku kufungua mlango gari likiwa linatembea”

Na Leah Kamala

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametoa malalamiko yao kuhusiana na tabia ya makondakta wa vyombo vya moto kutofunga milango ya gari pindi gari linapokuwa katika mwendo.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa milango ya gari isipofungwa huweza kusababisha mizigo kudondoka pamoja na kutokea kwa ajali.

Sauti za wananchi

Akitoa elimu kwa baadhi ya madereva na makondakta wa magari stendi ya zamani Mrakibu wa polisi na mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Mpanda mkoani Katavi Efeso Sukunala amesema kuwa ni marufuku kufungua mlango wakati gari likiwa kwenye mwendo hivyo hatosita kuwachukulia hatua wale wote watakaokaidi.

Sauti ya Sukunala

Kwa upande wao baadhi ya madereva na makondakta wamelishukuru jeshi la usalama barabarani kwa elimu waliyoitoa na kuahidi wako tayari kufuata sheria za usalama barabarani.

Sauti ya madereva na makondakta

Usalama barabarani ni jukumu letu sote hivyo mamlaka zinazohusika ziimaarishe ukaguzi na utekelezaji wa sheria ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya watu.