Mpanda FM

Madada poa 17 watiwa mbaroni Katavi

18 July 2025, 11:25 am

Kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Kaster Ngonyani. Picha na Samwel Mbugi

” Tumekamata vijana 3 na madada poa 17 na tumewapeleka mahakamani”

Na Samwel Mbugi

Jeshi la polisi mkoani Katavi limefanikiwa kukamata madada poa 17 na vijana 3 waliokuwa wakijihusisha na matukio ya kihalifu.

Hayo yamesemwa na kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi SACP Kaster Ngonyani wakati wa kipindi cha kumekucha Tanzania ambapo amesema  kuwa doria iliyofanyika hivi karibuni katika mtaa wa Tanzanite maarufu mtaa wa fisi uliopo kata ya Majengo walibaini uwepo wa biashara za ngono.

Sauti ya Ngonyani

Kamanda Ngonyani amesema kuwa uwepo wa madada poa katika eneo hilo umekua kichocheo cha kufichwa kwa  vitendo vya uhalifu na wahalifu.

Sauti ya Ngonyani

Katika hatua nyingine kamanda Ngonyani amesema kuwa jeshi la polisi mkaoni hapa wamejipanga katika kipindi hiki cha kuelekea uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu.