Mpanda FM
Mpanda FM
26 June 2025, 8:47 am

Mahali ulipopumzishwa mwili wa Silavius. Picha na Leah Kamala
“Ni tukio ambalo haulitegemei linatokea katika utafutaji”
Na Leah Kamala
Kijana mmoja mwendesha pikipiki ya magurudumu matatu maarufu kama bajaji kata ya Nsemulwa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Silavius Nestory Kameme ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya Milupwa manispaa ya Mpanda mkoani katavi na watu wasiojulikana.
Wakielezea tukio hilo mashuhuda wamesema kuwa wemeshtushwa na kuumizwa hivyo wameliomba jeshi la polisi kuweka ulinzi.
Aidha katibu wa waendesha bajaji amesema kuwa kama vingozi wameweza kuweka mikakati itakayowasaidia kupunguza matukio hayo.
Kwa upande wa ndugu wa marehemu, kaka wa marehemu Ladislaus amesema kuwa tukio hilo limetokea eneo la milupwa.