Mpanda FM

Wazazi/walezi msiwatelekeze watoto

14 June 2025, 12:15 pm

Meneja wa Mpanda radio FM Denis Mkakala. Picha na Samwel Mbugi

“Tumekuja kuwasalimia watoto na kuwaletea zawadi”

Na Anna Mhina

Wazazi na walezi wa mkoa wa Katavi wameshauriwa kuhakikisha wanasimamia misingi ya malezi bora ya kulea watoto na si kuwatelekeza.

Hayo yamesemwa na meneja wa Mpanda radio FM Denis Mkakala walipotembelea kwenye kituo cha kulea watoto yatima na walio katika mazingira magumu cha mtakatifu Yohana wa pili ikiwa ni mwendelezo wa kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika.

Sauti ya meneja Mpanda FM

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda ambaye ni afisa maendeleo ya jamii Joshua Sankala amekipongeza kituo cha Mpanda radio kwa kushiriki vema katika kuwaelea watoto.

Sauti ya afisa maendeleo ya jamii

Naye mkurugenzi wa kituo cha Mt. Yohana wa pili sister Rose Sungura ameeleza furaha yake na kuthamini mchango uliotolewa na Mpanda radio FM.

Sauti ya sister Rose

Ikumbukwe kuwa maadhimisho ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka ifikapo June 16 ikiwa ni kukumbuka watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia huko Afrika kusini mwaka 1976.