Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 5:30 pm

‘Amewaasa wananchi kuachana na matumizi ya earphone ili kuepukana na changamoto za uchovu wa masikio,maumivu ya kichwa.‘
NA Rhoda Elias -Katavi
Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda mkaoni Katavi wameiomba serikali kutoa elimu zaidi juu ya madhara yanayoweza kutokana na matumizi ya earphone kwa muda mrefu.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM wananchi hao wamesema kuwa wanatumia earphone Kwa mazoea pasipo kutambua madhara yanayoweza kujitokeza.
Gabriel Elias ni mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Town clinic amewaasa wananchi kuachana na matumizi ya earphone ili kuepukana na changamoto za uchovu wa masikio,maumivu ya kichwa.
Matumizi ya earphone kwa muda mrefu yanaweza kusababisha matatizo ya kusikia, kuathiri mfumo wa neva,na kuongeza hatari ya kupata kansa kutokana na mionzi ya kifaa kinachotumika.