Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 3:12 pm

Ulinzi shirikishi katika mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio manispaa ya Mpanda mkoani Katavi umetajwa kuwa moja ya njia inayosaidia kutokomeza matukio ya kihalifu
Wakizungumza na Mpanda Redio FM baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mpadeco wamesema kuwa ulinzi shirikishi umesaidia kutokomeza matukio ya mwizi katika mtaa huo huku wakiomba serikali kuhakikisha watu wanaofanya shuguli hiyo ya ulinzi kuwapatia vifaa na vitambulisho ambavyo vitawasadia katika majukumu yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio Ivo chambala amesema kuwa hadi sasa kuna kesi tatu ambazo zimefikishwa kituo cha polisi kupitia ulinzi shirikishi na kuwaomba wananchi kuwa makini nyakati za mchana kwani yapo baadhi ya matukio ya wizi ambayo yanafanyika nyakati hizo na yatari yameripotiwa.
Aidha chambala amewaomba wananchi kuendelea kuchangia fedha kwa ajili ya ulinzi shirikishi ambapo mtaa huo wa Mpadeco unajumla ya kaya 674.